MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameliomba Bunge
kurekebisha sheria za Magereza katika vikao vyao vinavyoendelea mjini
Dodoma.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Lulu
alisema kutokana na kukaa huko kwa mwaka mmoja, ameona mambo mengi
ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.
“Unaweza ukamkuta mfungwa
ana miaka zaidi ya 20 lakini hajawahi kufikishwa mahakamani wala
kuulizwa chochote kutokana na kitu ambacho kimempeleka hapo, kiukweli
hata kama ana makosa haiwezekani kumkalisha miaka yote hiyo pasipo
kusikilizwa,” alisema.
Alisema yeye amekaa huko kwa muda mfupi lakini
amepata shida sana kuyazoea mazingira hayo, kwani huwezi kuishi kama
nyumbani, hivyo ni vizuri ukiwekwa utaratibu mtu anasomewa kesi yake kwa
muda gani.
Lulu alilazimika kukaa gerezani kwa muda huo kwa tuhuma
za mauaji ya aliyekuwa nguli wa filamu nchini, Steven Kanumba,
aliyefariki dunia nyumbani kwake Sinza Vatican Aprili 7, mwaka jana