Taarifa za kipa nyota, Juma Kaseja
kutua Yanga zimewachanganya watu wengi. Ingawa zimekuwa hazina uhakika,
lakini Salehjembe imepata taarifa za uhakika kwamba mchana huu ndiyo
amemalizana na Yanga. Lakini bado watu wamekuwa wakihaha kutaka kujua
kuhusiana na suala hilo.
Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema; “Sitaki kulizungumzia kwa sasa, kama kuna walioandika sawa, lakini kumalizana
kwetu na Juma ni leo (Alhamisi).
Tulimpa mkataba, anao yeye, hivyo tutakutana na kumalizana leo na
tumegawanya makundi mawili, moja litakuwa uwanjani katika mechi dhidi ya
Oljoro na lingine katika ishu hiyo ya Kaseja.”
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KOCHA
Muingereza, Stewart John Hall ameamua kujiuzulu kufundisha klabu ya
Azam FC baada ya kukubaliana na wamiliki wa timu hiyo na leo hii
amewaaga wachezaji wa timu hiyo.
Stewart
aliwaaga wachezaji na benchi la Ufundi mara tu baada ya mchezo wa
mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina
ya timu hiyo na Mbeya City ulioisha kwa sare ya kufungana mabao 3-3
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.(P.T)
“Ni kweli nimewaaga wachezaji na
wenzangu katika benchi la Ufundi, nimewaambia imebidi niondoke kwa
sababu nimepata kazi sehemu nyingine. Lakini pia wamiliki wa timu
wameridhia niondoke na ninaondoka vizuri, nawatakia kila heri,”alisema
Stewart alipozungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii.
Hii
inakuwa mara ya pili, Stewart kuondoka Azam, baada ya awali Agosti
mwaka jana kuondolewa kiasi cha mwaka mmoja tu tangu aajiriwe akitoka
kufundisha timu ya taifa ya Zanzibar.
Stewart
alifukuzwa baada ya kuiwezesha Azam kushika nafasi ya pili katika Ligi
Kuu na Kombe la Kagame, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati pamoja na
kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi na nafasi yake ikachukuliwa na
Mserbia, Boris Bunjak.
Hata
hivyo, baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu uliopita, Stewart
aliyehamia Sofapaka ya Kenya, alirejeshwa Azam kufuatia kutimuliwa kwa
Mserbia, Bunjak.
Stewart
akarudia kuipa nafasi ya pili Azam katika Ligi Kuu na kuipa Kombe la
Mapinduzi pamoja na kuiwezesha kutwaa taji la Ngao ya Hisani, michuano
iliyofanyika mjini Kinshasa, DRC, Desemba mwaka jana.
Bado
haijajulikana sasa Azam itaangukia mikononi mwa kocha gani, ikiwa sasa
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu umemalizika na wachezaji wanakwenda
mapumzikoni.
Stewart ni kocha
wanne kuondolewa Azam tangu ianze kucheza Ligi Kuu msimu wa 2007/2008
baada ya Wabrazil Neider dos Santos na Itamar Amorin na Mserbia Bunjak.
Azam
imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ikiwa katika nafasi ya pili
kwa pointi zake 27 sawa na Mbeya City, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga
SC wenye pointi 28.
Source: http://www.wavuti.com