www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA Karama Nyilawila amewataka
mabondia wa Tanzania kuacha imani za kishirikina na badala yake wafanye
mazoezi ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana, Nyilawila alisema hapendezwi na vitendo hivyo kwani vinauwa
viwango vya michezo nchini. Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nawasihi waachane na imani za
kishirikina kwani wanapokwenda huko huishia kupigwa kwa KO ila naamini
wakizingatia mazoezi yatawasaidia kufanya
vema,”alisema. Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia
kushinda pambano lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na
badala yake jitihada zake binafsi ulingoni ndizo zitakazomfaa. Alisema
watu wasitafute mchawi aliyesababisha Tanzania isifanye vema kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa wakiamini imani hizo.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika
mazoezi makali chini ya meneja wake Seleman Zugo na kwamba amejipanga
kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za
mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa K,O ya raundi
ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila ‘Super D’ uliofanyika
NOVEMBA 10 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba