‘Friends again’, ni maneno yaliyoandikwa na Amani Joachim (Chief
Operations Officers wa B’Hits), kwenye ukurasa wake wa facebook na
kupost link yenye picha inayowaonesha AY, Mwana FA, na Hermy B wakiwa
kwenye picha moja.
Wengine kwenye picha hiyo ni Fid Q, Carol Ndosi na Arthur.
Picha hiyo imepigwa usiku wa kuamkia leo (November 29) inamuonesha
Producer wa ‘Habari Ndiyo Hiyo’ Hermy B baada ya kumwagia ndoo ya maji
katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Leo mchana Hermy B amepost picha akiwa na FA uwanja wa ndege wa J.K na kuandika ‘Bday continues’.