Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani.
Kinyanganyiro
cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013
kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1.
Mashindano
haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali
wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na
Snura.
Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya
washiriki watano ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel
Msuya,Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha
majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth
Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho.
Katika
round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq
Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na
kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana.
CREDIT: millardayo.com