Wakati baadhi ya wasanii wa kiume wakichachamaa kurekodi nyimbo zao
wakishirikiana na wanamuziki wakubwa wa kimataifa(kolabo), msanii wa
kike katika muziki nchini Shaa, amesema kuwa hawezi kufanya jambo kama
hilo na staa yeyote wa nje bila kuwa na hakika kwa manufaa upande wake.

Kupitia mahojiano na Starehe mwanzoni mwa wiki, Shaa ambaye jina lake halisi ni Sarah
Kaisi anaeleza kuwa wasanii wengi nchini wamekuwa wakiacha kufanya
muziki utakaowanufaisha na kukimbilia kurekodi na wasanii wakubwa, huku
wakipoteza fedha nyingi ambazo wangewekeza katika muziki wa hapa
nyumbani na kufaidika zaidi. Endelea…

Starehe: Wasanii wengi sasa wanafanya kolabo za kimataifa, vipi upande wako una mpango gani mwaka huu?
Shaa: Siwezi kufanya kolabo na staa yeyote wa
kimataifa, mimi nipo kibiashara zaidi na ni ngumu kwangu kwa sababu
nahitaji kufanya muziki nipate fedha. Hizi kolabo za kimataifa unajikuta
ukimlipa pesa mhusika huku wewe ukiingia gharama ya kusafiri huko na
kurekodi. Kama unavyojua, inachukua muda na gharama kubwa, nahitaji
kufanya kitu ambacho nitafaidika nacho na siyo kunipotezea fedha.

Starehe: Wasanii wa kiume wamejitahidi kufanya kolabo na mastaa wakubwa wa nje unadhani wanafaidika katika hilo?
Shaa: Inategemea, lakini asilimia kubwa kolabo hizo ni za kulazimisha
na kupoteza pesa, siyo za kuuza au kumwingizia kipato mhusika.
Unatakiwa ufanye kolabo, kisha upate shoo kubwa za kurudisha gharama
uliyotumia. Lakini nionavyo mimi nyingi ni za kutafuta ujiko tu, siwezi
kufanya kolabo na D Banj kisha isiniingizie chochote.

Starehe: Wanamuziki wa kike wana nafasi katika soko la sanaa hapa nchini?
Shaa: Wanamuziki wa kike tuna nafasi kubwa zaidi.
Hii ni tofauti na wenzetu wa kiume, lakini tunashindwa kuitumia hiyo
nafasi, Tunapaswa kujiweka kibiashara zaidi, lakini wengi wanauza sura
tu na kulazimisha muziki. Muziki unataka kujipanga na kujinoa kila
wakati, lakini walio wengi wanaimba kwa mazoea na hawataki kubadilika.

Starehe: Unadhani nini kinasababisha wasanii wa kike kuibuka na kupotea sokoni baada ya muda mfupi?
Shaa: Ubunifu ni suala nyeti lenye matokeo chanya
siku zote, lakini wengi hawana muda huo na wanashindwa kuchukulia muziki
kama kazi. Mtu akiwa staa anajiendeleza katika mambo mengine na siyo
kuwa bize na muziki uliompa nafasi ya juu. Sasa mtu anaimba kila siku
hana mabadiliko, muziki ni kama chakula, inafikia hatua kinamkifu mtu,
au kama Big G utamu ukiisha unaitema. Tofauti na wenzetu Ulaya,
ukiangalia kila albamu ya mwanamuziki Beyonce au Rihanna ina ladha
tofauti na sauti yenye upekee.

Starehe: Hii ndiyo sababu iliyokufanya ukabadili staili ya uimbaji wako?
Shaa: Ndiyo, katika uimbaji wangu sikuegemea sehemu
moja, siyo kwamba siwezi kufanya, bali mimi ni msanii, lazima
nibadilike. Ndiyo maana nimeweza kuimba Kwaito, Mduara na ninaweza kuja
na muziki wa Injili pia. Hii haitamaanisha kwamba nimeingia kwenye
muziki huo moja kwa moja, mimi ni msanii mwenye uwezo wa kubadilika
kutokana na wakati.