![rivaldo d2e7d](http://www.mjengwablog.com/images/11/rivaldo_d2e7d.jpg)
MSHINDI wa Kombe la Dunia na gwiji wa
Brazil, Rivaldo ameweka historia baada ya kuonyesha picha akiwa na
mwanawe uwanjani anayetumia jina la baba yaje huyo.
Rivaldo, mwenye umri wa miaka 41,
aliingia uwanjani akitokea benchi wakati Mogi Mirim wakitoa sare ya 1-1
na XV de Piracicaba katike mechi ya ligi ya jimbo la Sao Paolo Uwanja wa
Romildo Ferreira.
Ilikuwa mara ya kwanza anacheza sambamba na mwanawe huyo mwenye umri wa miaka 18, Rivaldo Junior.
Kinda Rivaldinho ana safari ndefu kama kweli anataka kufuata nyayo za baba yake, aliyejipatia umaarufu mkubwa kwenye soka.
Katika mataji, Rivaldo ameshinda tuzo
ya Mwanasoka Bora wa Dunia maarufu kama Ballon D’Or mwaka 1999 katikati
ya miaka yake mitano ya kuichezea Barcelona ambayo alishinda mataji ya
UEFA Super Cup, mawili ya La Liga na Kombe la Mfalme.
Aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la
Dunia mwaka 2002 kabla ya kwenda kuongeza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya
akiwa na vigogo wa Italia, AC Milan.
Rivaldo, ambaye pia amechezea Santa
Cruz, Corinthians, Palmeiras, Deportivo La Coruna, Cruzeiro, Olympiacos,
AEK Athens, Bunyodkor, Sao Paulo, Kabuscorp na Sao Caetano, alirejea
kwa mara ya pili Mogi Mirim Desemba mwaka jana ambako aliibukia kisoka.
Pia ni rais wa klabu hiyo kwa sasa. Chanzo: binzubeiry