![Beyoncé Knowles](http://ia.media-imdb.com/images/M/MV5BNTcxMDgwNTIyNV5BMl5BanBnXkFtZTcwODg0MTg0OQ@@._V1_SX99_CR0,0,99,99_AL_.jpg)
Ni mrembo mwenye kipaji cha hali ya juu katika tasnia ya muziki na uigizaji, pia ni mama wa mtoto mmoja. Ni Beyonce Knowles, mrembo ambaye amesumbua sana kwa kibao cha Drunk in Love alichomshirikisha baba wa mtoto wake Jay Z.
Kwa sasa Beyonce anaachia ngoma nyingine kali iitwayo “Pretty Hurts” katika mdundo huo amezungumzia jinsi ambavyo fasheni zinawaumiza watoto wa kike akili, hasa pale wanapojaribu kufanya chochote ili mradi tu waende sawa na viwango vya urembo. Akiongea katika clip ya behind the scene ya video ya wimbo huo, Beyonce anasema “baadhi ya vitu ambavyo kina dada wanavifanya ili kuonekana wako katika viwango vya urembo, huwa vinaniumiza roho”