KLABU
ya Yanga SC imewataka wanachama wake, wapenzi wa soka na wadau kwa
ujumla wasikatishwe tamaa na kuhama kwa wachezaji wake, Mrundi Didier
Kavumbagu na mzalendo Frank Domayo kwenda Azam FC, kwani uongozi
umepanga kuboresha kikosi kwa kusajili wakali wengine.
Taarifa
ya Yanga SC kwenye tovuti yao imesema kwamba wachezaji hao wamehama kwa
mapenzi yao wenyewe, kwani walikwishakubaliana na uongozi kila kitu juu
ya kuendelea kuitumikia Yanga kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa
wamejiunga na Azam.
“Yanga
tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama kanuni
za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika wachezaji Haruna
Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio watakaoendelea, hivyo
uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu zitakazotumika kwa
msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali
uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao tangu
mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba yao
ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao
2014/2015.
Didier
Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni waliongea
na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya kuweka
sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo yote ya
msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya usajili
wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la Bagamoyo
linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu
Uongozi
wa Yanga uliandikia TFF barua mapema kuomba kupewa mwongozo wa kanuni
zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa msimu mpya
kufuatia Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu inapasa kuwa
na wachezaji watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga haujapata
majibu juu ya utaratibu utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu ijayo.
Hivyo
makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na uongozi wa
Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi
zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni
na katika hali ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini
kuichezea timu ya Azam FC.
Kuhusu
Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia alikuwa katika
makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013, alikubaliana na
uongozi juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia ilikuwa ni kuweka
sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo alisema hawezi kusaini mpaka
siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie wakala wake na ahadi hiyo
iliendelea kwa muda wa mwaka mzima kabla ya jana kusikia ameshasaini
timu nyngine.
Habari
hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans
lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walisindwa kuwa wakweli kwa
viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango yao ya kuondoka, hivyo
uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini wachezaji wanaonekana
hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga SC.
Taarifa
kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na ripoti ya kocha
mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa hivi karibuni baada
ya benchi la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na kuafikiana mipango
ya msimu ujao.
Aidha
uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na washabiki
wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani Yanga bado
ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea kuboresha kikosi
chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans katika usajli wa msimu
ujao,” imesema taarifa hiyo.

![]() |
Atabomoa benki? Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji ndiye tegemeo la fedha za usajili na uendeshaji timu kwa ujumla |