Sababu ya dada wa Beyonce anayejulikana kwa jina la Solange Knowles kumdunda shemeji yake Jay-Z haijawekwa wazi mpaka sasa tangu tukio hilo litokee usiku wa kuamkia jana. Tukio hili la kushangaza lilitokea huko Met Gala baada ya Jay Z, Beyonce na Solange kutoka katika hoteli ya Standard Hoteli jijini New York. Video inaonesha Jay Z, Beyonce na Solange wakiingia katika lifti na ghafla Solange akamcharukia Jay Z na kuanza kumshambulia.
Mwamuzi wa pambano hili alikuwa baunsa wa Jay Z ambaye alikuwa akimzuia Solange ambaye alikuwa akijitutumua kurusha mateke. Kitu cha kuvutia kuhusu Jay Z ni kwamba mbali na kupaniki kwa shemeji yake huyo, yeye aliishia kuzuia mashambulizi hayo bila kujibu wala kuonesha hasira. Wakati yote haya yanaendelea Beyonce hakujishughulisha kabisa na mpambano huu.