Kwa wapenzi wa soka la Uingereza leo inabidi wachague kushabikia Arsenal au Hull City kwani hakuna mchezo mwingine mkubwa zaidi ya huo baada ya kumalizika kwa ligi kuu.Kwa familia ya Arsenal, huu ndio mchezo pekee ambao unaweza kuwaongezea muda wa kuongea au kuwamaliza kabisa wasiwe na cha kusema. Kwa mara ya mwisho Arsenal walishinda kombe hili wakiifunga timu ambayo ni mahasimu wao wakubwa Manchester United mwaka 2005.
Kwa upande wa Hull City wao wanacheza fainali ya kwanza katika kombe hilo.
Fainali hiyo itapigwa katika uwanja wa Wembley mishale ya saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Leo shabiki mwenzangu itakubidi utazame mpira huku unasikiliza Redio upande mwingine kukwepa kukosa utamu wa Barcelona na Atletico Madrid.
Katika mchezo huo ambao unazikutanisha timu inayoongoza ligi hiyo Atletico Madrid na timu inayoshika nafasi ya pili Barcelona tunatarajia kuona kandanda bora kabisa huku Barcelona wakihitaji ushindi ili kubeba ndoo ya Laliga kule Atletco Madrid wakihitaj sare ya aina yoyote ili kushinda kombe hilo.
Mashabiki wa Barcelona wanahitaji kuona timu yao inalipa kisasi cha kutolewa katka ligi ya Mabingwa na wapinzani wao wa leo Atletico Madrid kwa kuwafunga na kutwaa kombe la Laliga. Atletico hawajashinda kombe la Laliga tangu mwaka 1996.
Huku Messi kule Costa ni saa moja usiku
Mchezo mwingine kabambe ni mchezo kati ya Real Madrid na Espanyol ambao mpaka tuna kupasha habari hizi tayari Madrid wanaongoza kwa bao 1-0.
Kule Ujerumani kuna mchuano wa Mabingwa wa Bundesliga na washindi wa pili ni Bayern Munchen dhidi ya Borusia Dotmund. Mchezo huu wa fainali ya kombe la DFB Pokal utapigwa mishale ya saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.