Kila binadamu hufurahi kuona binadamu mwenzake anamkubali toka moyoni. Hata ingekua mimi au wewe ungefarijika pale endapo mtu angeulizwa swali kuhusu ni nani anampenda katika jamii ambayo wewe upo na akaishia kukutaja wewe.
Mwanadada mrembo na mkali wa muziki nchini Nigeria ambaye pia ametajwa kuwania tunzo za MTV MAMA 2014 aliulizwa swali na shabiki katika ukurasa wa Twitter wa MTV kuwa ni mwanamuziki gani anamkubali kutoka Tanzania?
Na Tiwa Savage hakusita kujibu kuwa ni kijana Diamond Platnumz. Wewe je, chaguo lako linafanana na Tiwa Savage?
![](https://pbs.twimg.com/profile_images/466563477184577537/ItZcU3eG_normal.jpeg)