Rapa kutoka maandishi matatu pande za kwa Obama amewekwa chini ya ulinzi baada ya kukutwa na jani la mmea wa bangi wakati wa ukaguzi katika uwanja wa ndege wa Texas. Mtandao wa udaku nchini U.S.A, TMZ umeripoti.
Staa huyo wa Black and Yellow alikumbwa na mkasa huo asubuhi ya jana Jumapili wakati akitarajia kusafiri kutoka El Paso kuelekea Dallas. Vyanzo vya kiusalama na sheria vimesema kwamba baada ya maafisa wa ukaguzi kugundua kuwa Wiz Khalifa alikuwa na chembechembe za ganja, walimpeleka rumande na baadae kumpeleka kituo kidogo cha polisi.
Polisi walithibitisha kuwa Wiz alikuwa na bangi isiyopungua nusu gramu na hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wa Wiz mwenyewe hakukoment kitu, ila ameweka picha inayomuonesha akiwa jela katika mtandao wa kijamii wa Twitter.