Waswahili huwa wanasema, “lisemwalo lipo” katika uhusiano wa masupastaa ambao watu wengi huutolea mfano kama moja ya mapenzi makini ulimwenguni ni kati ya Jay Z na Beyonce.
Lakini kuna tetesi kuwa Beyonce anachepuka na bodyguard wake aitwae Julius De Boer.
Chanzo cha habari kinadai kuwa Jay Z amekuwa akimpinga sana bodyguard huyo na kutaka afukuzwe lakini Beyonce amekuwa akimtetea Julias ambaye amekuwa baunsa wake tangu mwaka 2009. Kisa hiki pia kinahusishwa na ugomvi kati ya J Z na Solange.