Picha iliyopigwa na wasanii wawili wa filamu ambao wametangulia mbele ya haki Adam Philip Kuambiana na Rachael Haule pamoja na mungozaji wa filamu hapa nchini Saidi Walley imeleta utata. Utata huo umekuja baada ya wasanii hao wawili kufariki ndani ya mwezi tu, kwenye hiyo picha anaanza Kuambiana anafuata Rachel na Muongozaji wa filamu hapa nchini Saidi Walle ambaye yupo hai, utata unakolezwa zaidi kutokana na kwamba umauti umewakuta kwa mtirirko huo huo alianza Kuambiana na sasa amefuatia Rachel, chanzo chetu cha habari kimebaini kuwa watu wa karibu wa Saidi Walle ambaye ndiye amebaki hai miongoni mwa waliokuwepo kwenye picha hiyo wanajiuliza Je? atafuata Saidi Walle kwa siku hizi za hivi karibuni? Picha hiyo ilipigwa 3/05/2012 wakiwa location wakati wakishoot filamu ya THE BOSS ambayo Adam Kuambiana na Rachel Haule walikuwa kama waigizaji na Saidi Walle akiwa kama mpiga picha na muongozaji.
Mtandao huu wa Taswirabongo ulifanya jitihada za kumtafuta director huyo na kufanikiwa kumdodosa kuhusu hili. Director huyo alisema tangu kilipotokea kifo cha Rachel marafiki, ndugu na jamaa wananiambia ninafuata na mimi siku si nyingi baada ya kuiona picha ambayo tulipiga mimi, marehemu Kuambiana na Rachel. “Mimi siogopi kwani yote ni mipango ya Mungu, hii imetokea tu wasione ajabu sana, inaweza ikatokea kwa mtu yeyote yule hapa duniani, kwa hiyo najiona kawaida tu”, alisema director huyo ambaye kabla ya kifo cha kuambiana alinusurika na kifo baada ya gari yake kupata ajali mbaya sana barabara ya Bagamoyo maeneo ya Boko.
Picha ya gari la Director Said Walley likiwa liharibika vibaya ajali hiyo ilitokea siku kadhaa kabla ya kifo cha Adam Kuambiana
Director Saidi Walley akiwa na Adam Kuambiana
Director Saidi Walley akiwa na Rachel Haule