Mexico wameichabanga Croatia kwa mabao 3-1. Mexico wamecheza mchezo huo wa kupimana nguvu wakiwa nyumbani.
Wafungaji wa magoli ya Mexico ni L. Montes dakika ya 33, M. Fabian dakika ya 69 kabla ya kipa wa Ecuador, M. Banguera kujifunga dakika ya 76.
Goli la kufuta machozi la Ecuador lilifungwa dakika ya 80 na J. Jaguar.
Katika mchezo huo mshambuliaji mahiri wa Mexico ambaye ni mfungaji wa goli la kwanza Lous Montes amepata majeraha yatakayompelekea kulikosa kombe la Dunia baada ya kuumia goti na kushindwa kuendelea na mchezo huo.
Italia wametoshana nguvu na Ireland kwa kutokufungana, ingawa italia pia wamepata pancha kubwa katika safari yao ya kuelekea Brazil baada ya kiungo mshambuliaji Riccardo Montolivo kuvunjika mguu katika mchezo huo.
Vijana wa Van Gaal, walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ghana, bao likifungwa na nahodha Robin Van Persie. Baada ya mchezo huo, kocha wa Uholanzi Louis Van Gaal alilalamika kwa kusema timu yake ilihitaji kudi.
Ureno wakicheza bila nahodha wao Christiano Ronaldo ambaye ni majeruhi,walishindwa kufurukuta nyumbani baada ya kutoa sare ya kutokufungana dhidi ya Ugiriki. Kocha wa Ureno Paolo Bento amesema timu yake imefanya vizuri bila Ronaldo.
Colombia wakiwa nyumbani walipata sare ya 2-2 dhidi ya Senegal. Colombia walitangua kupata mabao mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji Teofilo Gutierrez ambaye aiifunga katika dakika ya 11 ya mchezo na Carlos Bacca akifunga goli la pili kabla ya kipenga cha kumaliza kipindi cha kwanza kupulizwa.
Senegal kupitia kwa mchezaji wao Moussa Konate walijipatia bao la kwanza dakika 2 tu baada ya kuanza kwa kipindi cha lala salama na bao lao la kusawazisha likifungwa dakika tano baadae kupitia kwa kiungo Cheikh Ndoye na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ubao kusoma 2-2.
Warusi wakiwa chini ya Fabio Capelo walishindwa kuonesha makucha yao baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Norway.Urusi ilikamata usukani wa mchezo baada ya Olegi Shatov kuipatia goli katika dakika ya 3 ya mchezo, goli hilo lilidumu mpaka dakika ya 77 ambapo Anders Konradsen alirudisha heshima ya Wanorwey. Kocha Fabio Capelo ameilalamikia timu yake kwa kushindwa kucheza katika kiwango alichotarajia na kushindwa kutumia nafasi ipasavyo.
Wawakilishi wengine kutoka Afrika, Algeria waliweka hai matumaini yao ya kufanya vizuri baada ya kuitwanga Armenia kwa mabao 3-1. Essaid Belkalem, Nabil Ghilas na Islam Slimani walifunga magoli hayo matatu katika ngwe ya kwanza ya mchezo huo.
Akitokea bench ndani ya kipindi cha kwanza Artur Sarkisov aliipatia Armenia goli la kufutia machozi dakika chache kabla ya filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza kupulizwa.
.
Uruguay bila mshambuliaji wao tegemezi Luis Suarez walichomoza na ushindi mdogo wa 1-0 dhidi ya Norwey Kaskazini bao likfungwa dakika ya 62 na Christian Stuani aliyetokea benchi.
Wawakilishi wengine wa Afrika katika michuano ya kombe la Dunia, Ivory Cost walisafiri hadi Bosnia ambako walicheza dhidi ya ya timu inayoundwa na Bosnia na Herzegovina. Ivory Cost ilipoteza mchezo huo kwa kupigwa goli 2-1 na wenyeji wo. Huku goli lao la kufutia machozi likifungwa na nahodha Didier Drogba katika dakika ya 90. Magoli yote mawili ya Bosnia na Herzegovina yalifungwa na mshambualiaji wa Man City ya Uingereza, Edin Dzeko dakika ya 17 na 53. Kocha wa Ivory Cost amesema timu yake ilipaswa kupoteza kufuatia madhaifu iliyoonyesha
Chile wamepata ushindi wa 3-2 dhidi ya mafarao wa Misri. Katika mchezo huo ambao Misri walisafiri mpaka Amerika ya Kusini, wenyeji walivutwa jezi hadi dakika ya 77 ambapo nyota wa mchezo huo Vargas aliipatia Chile goli la ushindi.
Mafarao walikuwa wa kwanza kung’aa kupitia kwa Mohamed Salah aliyefunga goli la kuongoza dakika ya 11 ya mchezo akifuatiwa na K Kamar dakika ya 16. Chile ilipata goli lao la kwanza kupitia kwa Diaz dakika ya 26 na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika matokeo yalikuwa ni Chile 1- Misri 2.
Kipindi cha pili wenyeji walicharuka na dakika ya 60 Vargasi alisawazisha kabla ya kuishindia Chile dakika ya 77. Alexis Sanchez wa Barcelona alikuwa chachu kubwa ya ushindi wa Chile kwani ndiye aliyepiga pasi za mwisho za magoli yote matatu.
Sanchez kulia |