Timu ya Taifa ya Tanzania imefuzu hatua ya awali ya michuano ya Mataifa huru barani Afrika baada ya kuilazimisha sare timu ya Taifa ya Zimbabwe.
Taifa Stars imepata matokeo ya 2-2 ugenini na kufuzu hatua ya awali kufuatia ushindi iliyoupata nyumbani wiki moja iliyopita.
Zimbabwe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 24 kabla ya Nadir Haroub canavaro kuisawazishia Stars dakika ya 28. Thomas Ulimwengu aliifungia Stars goli la kuongoza dakika ya 46 na Zimbabwe kusawazisha dakika ya 56.
Katika hatua ya pili Tanzania watapambana na Msumbiji.