Manchester United itasikiliza dau kwa timu inayotaka kumnunua kiungo wake Maroanne Fellaini, na wapo tayari kumuuza kwa pauni milioni 15, licha ya David Moyes kumnunua kwa pauni milioni 27 msimu uliopita (Times), rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amepuuzia taarifa zinazomhusisha winga Lorenzo Insigne kwenda Arsenal (Evening Standard), Jose Mourinho amefutilia mbali nia ya Real Madrid kumsajili Ramires (Daily Star), Arsenal wanajipanga kumchukua beki wa kulia wa Southampton, Callum Chambers, kuziba pengo la Bacary Sagna (Daily Mirror), mshambuliaji wa Atlètico Madrid Diego Costa amesema uhamisho wake wa pauni milioni 32 kwenda Chelsea uko karibu kukamilika (Metro), hatua ya Manchester United kumsajili beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw iko mashakani baada ya Louis van Gaal kuanza kumtazama Jordi Alba wa Barcelona (Daily Express), QPR wanafikiria kumfanya beki wa kati wa zamani wa Man U, Rio Ferdinand kuwa mchezaji anayelipwa zaidi na klabu hiyo kwa kumpa pauni 80,000 kwa wiki (Guardian), meneja wa Napoli Rafael Benitez anataka kumsajili Jermaine Pennant, ambaye alikuwa naye Liverpool (Daily Mirror). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios!
Credit: Salim Kikeke