RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Mainzi ni kama ameridhia
mchakato wa uchaguzi wa Simba SC uendelee, lakini tu ameshindwa kuweka
wazi.
“Kwa
ustawi wa soka ya Tanzania, naamini maelewano yatapatikana,”amesema
Malinzi akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya
TFF, makutano ya mitaa ya Garden na Ohio, Dar es Saalaam.
Waandishi
wa Habari walitaka kujua kama ameruhusu zoezi la uchaguzi wa Simba SC,
liendelee au la kufuatia kauli ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa
klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage juzi.
Rais Malinzi akizungumza katikati |
“Namshukuru
Mwenyekiti wa Simba SC, Rage na Kamati yake ya Utendaji tangu juzi
wamekuwa katika mawasiliano na mimi kwa nia nzuri tu, wakiomba uchaguzi
usisimamishwe. Nami nimeruhusu mgombea mmoja aliyekata rufaa yake Kamati
ya Rufani ya TFF, kesi yake isikilizwe leo.
Mazungumzo
yanaendelea, na yataendelea baada ya kikao cha leo, naamini hakuna
kitakachoharibika, ufumbuzi utapatikana,”amesema Malinzi.
TFF
ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Simba SC hadi hapo klabu hiyo
itakapounda Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya kimaadili
kuelekea uchaguzi huo.
Malinzi
alisema mwishoni mwa wiki kwamba Simba SC inatakiwa kuwa imekwishaunda
Kamati ya Maadili hadi kufika Juni 30, mwaka huu, hatua ambayo alidai
imefuatia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa
baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi
alisema kwamba baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza
malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo,
ambao awali ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Aliagiza
kwa sasa Kamati ya Utendaji ya Simba SC iliyopo madarakani chini ya
Mwenyeiiti wake, Rage itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato
wa uchaguzi utakapokamilika.
Lakini
mwanzoni mwa wiki, Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC ilimpinga Malinzi,
ikisema TFF haina mamlaka ya kusimamisha uchaguzi huo na Jumatatu, Rage
akamuomba raisi huyo wa TFF aache mchakato wa zoezi hilo uendelee kwa
manufaa ya Simba SC