Vyombo vingi vya habari vimekuwa vikiripoti juu ya mahusiano ya masupastaa vijana kabisa katika tasnia ya burudani, Justin Bieber na Selena Gomez. Mastaa hao ambao waliwahi kushibana vilivyo katika ulingo wa mapeenzi na baadae kumwagana, wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kurudiana. Taarifa hizo zilizagaa baada ya wawili hao kuonekana sehemu tofauti za kujivinjari, lakini ujweli umekuwa wazi baada ya Bieber mkali wa “Confident” kuonekana na mrembo mwingine ambaye ni mwanamitindo Yovanna Ventura.
Justin Bieber na Yovanna wamekuwa wakipokezana kuweka picha kwenye mitandao katika hali ya kuthibitisha kuivana kimahaba. Picha ya hivi karibuni ina muonesha Bieber akiwa ameuzungusha mkono wake katika kiuno cha Yovanna, na nyingine inamuonesha Yovanna akiwa amemshikilia kiuno Bieberkwa nyuma.
Kwa upande wa Selena Gomez, yeye amekuwa mtu wa kuweka picha ambazo yuko na marafiki zake wa kike na kuandika maneno ambayo mashabiki wanahisi yanamlenga babito wake wa zamani (Justin Biebe)