![0718_nelson_mandela_leo_dicaprio](http://ll-media.tmz.com/2014/07/18/0718-nelson-mandela-leo-dicaprio-2.jpg)
Mwigizaji nguli Duniani Leonardo Dicaprio leo ametoa dukuduku lake kuwa picha aliyopiga na hayati Nelson Mandela iliibiwa na anfanya jitihada za kuhakikisha anaipata tena. Picha hiyo (juu) aliipiga wakati anashuti filamu ya “Blood Diamond” huko nchini Afrika ya Kusini na anachoamini Dicaprio ni kwamba picha hiyo iliibwa na tayari ameshaanza kumtumia mwanasheria wake ili kuifuatilia kampuni ambayo inazalisha picha hizo na kuziuza. Kampuni ijulikanayo kama Moment in Time ndiyo inajihusisha na uzalishaji wa hiyo na kuuza kwa dola 25000 za Marekani.
Hata hivyo mtandao wa TMZ umefanikiwa kumpata mmiliki wa Moment in Time na ameeleza kuwa kampuni yake iliinunua picha hiyo mwezi uliopita na haoni sababu ya kutouza kopi.
Haya yameibuka wakati Dunia inakumbuka mchango wa hayati Nelson Mandela, baada ya kuteuliwa kwa tarehe 18 ya mwezi Julai kuwa siku rasmi ya kukumbukwa kwa raisi huyo wa zamani wa Afrika Kusini na mwanaharakati wa haki za binadamu ulimwenguni. Haya ni maadhimisho ya kwanza tangu kifo cha Mandela Desemba 5, 2013.