Jarida la MEN’S HEALTH limemtangaza nyota wa Real Madrid ambaye pia anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora ulimwenguni kuwa Binadamu mwenye afya nzuri zaidi kati ya Binadamu wote wanaoishi.
Mkali huyo wa kulisakata kabumbu kutoka nchin Ureno amepamba jalada la Jarida hilo akiwa kifua wazi na kwa kutazama tu mwili wake, ni ngumu kubisha kauli hiyo ya MEN’S HEALTH.
Jarida hilo limetoa baadhi ya vitu walivyozingatia kabla ya kumvisha Ronaldo sifa hiyo, na baadhi ya vigezo ambavyo wametaja ni pamoja na:
Uwezo wa kukimbia umbali mrefu: Ronaldo hukimbia zaidi ya maili sita (6) kwa mchezo mmoja.
Kiwango cha mafuta mwilini (fat) ni kidogo, misuli yake imejengeka vyema.
Nguvu: Ronaldo ana nguvu ambayo inamuwezesha kupiga mpira umbali wa maili 80 kwa saa. Hii imetajwa kuwa sababu ya Ronaldo kufunga mipira mingi ya adhabu maarufu kama free kick.
Kasi ya kutumia akili na kufanya maamuzi ya haraka uwanjani pia ni moja ya vitu ambavyo vinambeba Ronaldo
Uwezo wa kuruka; Kwa mujibu ya jarida hilo Ronaldo ana uwezo wa kuruka inchi 31 kwenda juu na hii inamfanya aweze kucheza kwa kichwa mpira ambao uko juu hadi umbali wa futi 8.5.
Tazama hapa video ya wakati akitengeneza picha za jarida hilo: