Mwigizaji mkongwe ambaye pia aliwahi kuwa mwanamitindo wa nchini Marekani Halle Berry ameibukia katika biashara ya kutengeneza perfume akitoka na perfume inayokwenda kwa jina la “The Wild Essence” ambayo imetengenezwa kwa mitishamba. Halle Berry ameisifia perfume hiyo ya kike huku akisema imetokana na mimea halisi.
“Napenda wazo la kutengeneza marashi yatakayomuunganisha mwanamke na mazingira halisi kupitia pafyumu”, alisema Berry.
Mwigizaji huyo mwenye miaka 48 ameingiza perfume ya sita sokoni zikiwemo za awali kama Exotic Jasmine, Closer, Pure Orchid na ambayo aliipa jina lake Halle perfume.
Mbali na biashara hiyo ya perfume na uigizaji, Halle Berry pia ni mama wa watoto wawili.