Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita.
Moja kati ya story zilizoshtua mashabiki wa soka duniani mwishoni mwa wiki hii ni ajali ambayo aliipata nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England David Beckham.
Becks alipata ajali hii wakati akiwa anatoka kumchukua mwanae Brooklyn toka kwenye mazoezi ya kila siku na timu yake ya Arsenal ambapo gari la Beckham aina ya Audi liligongana na gari nyingine ndogo na kupelekea staa huyu kupata jeraha kwenye bega lake japo halikuwa jeraha kubwa sana.