Baada ya mwanadada mdau wa filamu nchini, Zamaradi mketema kufunguka yake juu ya filamu za bongo – bongomovies,
hatimaye mwigizaji mkongwe nchini Jacob Steven – JB ameamua kuandika
haya yafuatayo hapo chini kuelezea baadhi ya mambo anayohoji Zamaradi
kama ifuatavyo.
“Kwako Zamaradi na wengine wote.
Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia
mema. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz na
waandaaji wa filamuU kwa kuthubutu kutengeneza filamu hizi katiks
mazingira magumu. Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha
bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.
Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo zinakatisha tamaa. Hebu tujiulize kwa nini wasomi wengi waliosomea filamuu UDSM na BAGAMOYO
hawafanyi filamu hizi? Wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata
hans pop walijaribu wakakimbia, kuna producer mkubwa hapa nchini JOHN RIBER ambaye ametengeneza filamuu kama NERIA na YELLOW CARD lakini naye ukimwambia njoo kwenye hizi filamu atakupa jibu.
Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filamu zetu na
stori lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filamu bongo
yanakatisha tamaa wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi
wamekimbia. Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji
kwa sasa kupitia JERUSALEM FILMS na ndio maana filamu nyingi natoa
nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera ya filamu yatafanywa
watatuwakilisha nje.
Kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kibwa sana. Tukumbuke SHARUK KHAN ni ‘actor’ tajiri2 dunian lakini filamu zake ni za kihindi. Hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na EAST AFRICA
kwanza huku tukiboresha, wasomi wa filamu msikimbie njooni tuanze wote
na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa
vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na mungu bila msaada
kutoka popote. Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filamu zetu.”
Alimaliza kwa kusema JB.
Source
http://www.bongomovies.com