Ikiwa ni tatizo la watu maarufu mbalimbali nje ya nchi na baadhi yao pia hapa ndani (offcourse juzi tumesikia juu ya Sugu), Suala hili kwa upande wa Ney limekaa tofauti kudogo ambapo kwa mujibu wake, Baby Mama Siwema pembeni ya sheria, hajawahi kufanya jitihada yoyote kumuona mwanae kuelekea kipindi cha nusu mwaka sasa.
Ney amesema, licha ya mama wa mtoto huyo kuwa na mawasiliano na ndugu zake wengine kutoka familia yake, kama mama anayetakiwa kumjali mtoto wake mdogo, hajawahi kusikia hata jitihada ya aina yoyote ya Siwema kujaribu kumuona mtoto, kitu ambacho akikifanya hapo baadaye, binafsi atamuona kuwa ni mnafiki.
Ney katika wakati huo huo anaendelea kukaza kwa upande wa kazi zake, akiwa na rekodi mpya kabisa ‘ngumu’ kuwachana wanaoenda kinyume na mstari kama kawaida yake, ikiwa imepatiwa jina Sina Muda.
–EATV