Mitandao mingi ya kijamii ilitapakaa habari za Drake kupigwa na mkongwe P Diddy na kupelekea kutenguliwa bega. Habari hizo zilitawala mitandao ya kijamii mwanzoni mwa wiki hii ingawa kati ya marapa hao wawili hakuna aliyezungumza chochote juu ya sakata hilo baadhi ya mapaparazi wamearifu kuwa chanzo cha sintofahamu hilo ambalo lilitokea Miami Beach inasadikiwa kuwa Drake kummendea mwanadada Cassie ambaye ni mpenzi wa P Diddy na pia P Diddy anamshutumu Drake kumwibia beat.
Baada ya kusemekana kuwa Drake amepelekwa hospitali kimya kingi kimetanda huku mashabiki wakiwa na hamu ya kusikia chochote kutoka kwa wawili hao.
Jumatano hii Drake ndiye alianza kufunguka instagram kwa kusema kuwa hajali maneno yanayozungumzwa ila anachojali ni jina lake kuendelea kung’aa. Isome hapa post yake
P Diddy naye amekaa kimya ingawa amepost picha hii hapa