WAKATI baadhi ya wasanii wakipewa masharti kuacha kuigiza pindi wanapoolewa, nyota wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’, amedai hata kama akiamua kuolewa na kuishi na mwanaume kamwe hawezi kuachana na tasnia hiyo kwani ndiyo iliyomfanya aishi maisha mazuri mjini.
Nisha alizungumza na paparazi wetu juzikati na kudai kuwa wanawake wengi wamekuwa maskini kwa kuwa wanashindwa kuendelea na kazi walizokuwa wakizifanya awali kutokana na kubanwa na wanaume ambao hawana malengo ya maisha.
“Sidhani kama atatokea mwanaume atakayesema eti acha filamu ndiyo uwe mke wangu, wapo ambao walileta ujinga huo na wakaishia njiani kwa sababu hawana jambo geni, maisha yangu yamejengwa na filamu na ndiyo kazi inayonipa kila ninachokitaka, siiachi,” alisema Nisha.
CHANZO; GPL