Wachezaji Jordan na Diego costa siku ya jumanne walitunishiana msuli kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la ligi uliofanyika Anfield na mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Mmoja wa wafanyakazi wa klabu ya Liverpool alimtenganisha kiungo huyo pamoja na mshambuliaji wa Chelsea wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Wachezaji hao hawakugombana bali walikuwa wanajibizana kwa maneno tu.
Mchezaji Henderson alikuwa anapinga kitendo cha Diego cost kumchezea faulu mchezaji Raheem Sterling wakati akielekea langoni mwa klabu ya Chelsea kusawazisha goli.