Muigizaji wa filamu hapa bongo na Mwanamitindo Jokate Mwegelo na Elizabeth Michael ‘Lulu”. hivi karibuni walishindanishwa kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini na Jokate Mwegelo kuibuka msindi kwa kumshinda mshindani wake ,Elizabeth Michael ‘Lulu”.
Mtandao mmoja wa hapa nchini umeendesha zoezi la kuweka picha zao kali zinazowaonesha wote wawili wakiwa na muonekano na picha kali huku wakiuliza nani zaidi ya mwenzake.Jokate ameibuka mshindi kwa kupigiwa kura tano huku watu wakimsifia kuwa ni wa kimataifa zaidi ambapo Lulu alionekana kupigiwa kura na mtu mmoja.
Akizungumzia ushindi huo Jokate aliwashukuru Watanzania kwa kumpenda na kumpa nafasi lakini aliwasihi kwa kuwaambia kuwa yeye aonavyo wote ni warembo.“Mimi naona sisi wote ni warembo, nawashukuru Watanzania walionichagua na kuniona nafaa,” alisema Jokate
Source: GPL