Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, anatarajia kuanza kutambulisha nyimbo zake mpya katika ziara yake nchini Marekani, Februari 13 hadi 15, mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wetu, Ommy Dimpoz amesema ziara hiyo itakuwa ya kwanza tangu mwaka huu uanze.
“Natarajia kuanza ziara yangu ya kwanza mwaka huu nchini Marekani”.
“Natarajia kuanza ziara yangu ya kwanza mwaka huu nchini Marekani”.
Amesema kuwa atafanya ziara ya siku tatu Marekani badaye atarejea nchini ili kuja kujiandaa na safari ya kurudi nchini humo maana ratiba yake inaonyesha Februari 21 atakuwa na shoo maalumu jijini New York.