MLEZI wa Klabu ya Bongo Movies, Catherine Ambakisye Mama Loraa amefunguka kuwa matatizo na mifarakano inayotokea ndani ya klabu hiyo ni kutokana na kukosa bodi ya ushauri.
Akilonga na Uwazi, Mama Loraa alisema wasanii mbalimbali ambao waliwahi kuiongoza klabu hiyo miaka ya nyuma ndiyo tatizo na kwamba Bongo Movies imekosa bodi inayotakiwa kushughulikia matatizo yanapotokea au kutoelewana kwa wasanii.
Bongo Movies imekosa bodi ya ushauri. Nimeshawahi kuwashauri mara kadhaa wachague bodi ambayo itakuwa inadili na mambo ya klabu sambamba na kutoa ushauri hasa linapokuja suala la kusimamia pesa na ugomvi unapotokea, alisema Mama Loraa.