Chama
cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania Bloggers
Network’ – TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho
kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji
wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania
wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa kuu kwa mwanachama ni
kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa
mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka
kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania
Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala
na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama mhitaji wa kujiunga
kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha
mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa
mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama
(utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/-
na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi
kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu
litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu
pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na
Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa wanachama wa mikoani
utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama
watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu
unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa
kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa
na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la
kujiunga uwanachama wa TBN.
Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda,
yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe),
Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam,
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya,
Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na
Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida),
Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya
Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya
Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).
Kwa
wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama
wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili
kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama
waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.
NB;- Kwa
watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy
hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft
coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN.
Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)