MwanaFA
amesema kuwa Staa wa Bongo,Diamond ana haki ya kutoa maoni na
malalamiko yake kuhusu tuzo za muziki za Kilimanjaro(KTMA) za mwaka huu.
Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena,alisema kilichomtokea Diamond
hata yeye kilimtokea wakati alipotoa wimbo wake wa ‘Bado Nipo Nipo
Kwanza’ ulifanya vizuri wakati huo lakini jina lake halikuwepo kwenye
tuzo hizo. ‘’Hata mimi nililalamika kama anavyolalamika Diamond lakini
niliwaandikia barua Killi wakaniita wakanielewesha kuwa ilikuwa ni
makosa ya kibinadamu nikaelewa,’alisema Mwana FA.
Pamoja na hayo
MwanaFA amesema amesikitishwa na wasanii kama Mo Music na Ommy Dimpoz
kutokuwepo kwenye tuzo hizo hasa video ya ngoma ya Ndagushima ambayo
ilifanya vizuri mwaka jana.