Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi aitwaye, Nagari, Staa wa Bongo Fleva, Linnah Sanga amepata mpenzi mpya aitwaye Williams Bugeme ’Boss Mutoto’ raia wa Uganda, ambaye hivi karibuni amechora ‘tattoo’ kwenye mwili wake yenye jina la msanii huyo.
Akizungumza na Clouds FM,Linnah alisema ilikuwa ni kit cha kushtukiza sana kwani mpenzi wake alimtumia sms kuwa anataka kumfanyia ‘surprise’ na afikirie ni kitu gani anataka kumfanyia alimjibu kuwa hajui ila amwambie tu.
‘’Alinitumia sms akaniambia ni ‘guess’ ni kitu gani anataka kunifanyia ‘surprise’ nikwambia mimi sijui basi akaniambia amechora tattoo yenye jina langu daah! Nilishtuka sana na pia nilikuwa na furaha sana,’’alisema Linnah.
‘’Unajua ni maamuzi magumu sana mtu kukuchora tattoo na mpaka anakuchora ujue basi ana mapenzi ya kweli na kama ni shabiki basi ni shabiki kwelikweli amezama kabisa,’’aliongeza Linnah.
Msanii mwingine aliyeweka rekodi ya kuchora tattoo ya jina la mpenzi wake na sura yake ni msanii wa Bongo Fleva,Nuh Mziwanda aliyechora tattoo ya mpenzi wake Shilole.
-udakuspecially