Baada ya wote wawili kuibuka washindi kwenye tuzo za MTV MAMA 2015 zilizotolewa Jumamosi iliyopita Durban, Afrika Kusini, Davido na Diamond wameweka wazi ujio wa collabo yao mpya.
Wakiwa na furaha huku wakiwa wamebeba tuzo zao mikononi mara baada ya tukio la utolewaji tuzo hizo kuisha, staa wa Nigeria Davido akiwa na Diamond ametoa ahadi ya collabo yao mpya.
Katika kipande cha video (hapo chini) Davido ametamka kwa kinywa chake:
“New F*ckin Diamond and Davido we gonna dropin next month, we do this f*ckn East Africa West Africa biggest artist we do this…we are uniting…” Wakati Davido akiyaongea hayo, Diamond alikua akiitikia “I’m telling you”.
Diamond aliibuka mshindi wa tuzo ya ‘Best Live Act’ na Davido naye aliibuka mshindi wa tuzo kubwa ya Best male ambayo pia alishinda mwaka jana.
Mpekuzi blog