50 Cent akiwa katika uwanja wa ndege wa Hearthrow jijini London akijianda na safari ya kurudi New York
Siku chache zilizopita msanii wa Hip Hop nchini Marekani 50 Cent, 40, alitangaza kufilisika kutokana na deni la dola mil 30 (zaidi ya tsh bil 62.4) analodaiwa kutoka katika vyanzo mbalimbali kushindwa kulilipa.
Lakini staa huyo mwenye ‘misifa’ kibao bado ameonekana katika kumbi tofauti za starehe akiwa amevaa mavazi ya bei ya juu huku akiwarushia fedha mashabiki wake jambo lililoibua maswali mengi miongoni mwawatu waliokuwa wakihoji kama kweli msanii huyo amefulia au alikuwa akijitafutia ‘kikii’.
Jumamosi iliyopita 50 Cent alionekana katika uwanja wa ndege wa Jijini London alipotoka kula ‘bata’ akiwa na begi la nguo la kampuni ya mavazi ya Louis Vuitton lenye thamani ya dola elfu mbili (tsh mil 4.16) akielekea zake New York huku tiketi yake ya ndege ikiwa ni ile ya first-class (daraja la kwanza).
Hivi sasa staa huyo mwenye vipaji kibao ameamua kujikita katika uigizaji ambapo kwasasa yupo katika uwaandaji wa filamu ya Southpaw aliyoigiza kama meneja wa mcheza boxer, Jake Gyllenhaal.