Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria, ametoa kali ya mwaka kwa kueleza kuwa, akishibishwa vilivyo na mume wake ‘chakula cha usiku’, haoni sababu ya kumsifia kupitia mitandao ya kijamii.
Mwanaharakati huyo amekuwa na tabia ya kumpa sifa kemkem mpenzi wake hasa akipewa mambo adimu ya ‘chakula cha usiku’ amedai kuwa haoni tatizo kufanya hivyo kwa kuwa kila mtu anajua akiolewa lazima apewe ‘chakula cha usiku’ na ashibe ndipo aifurahie ndoa.
“Mi sioni ajabu jamani kwa sababu ni vitu vya kawaida kabisa, nani asiyejua tumetoka kwa wazazi wetu kwa ajili ya kufuata ‘chakula cha usiku?’ Kwa hiyo sioni hatari kwa kweli, nitaendelea kumsifia mume wangu atakaponipa furaha,” alisema Joyce.