Msanii wa Mziki na Filamu hapa Bongo Hemed Suleiman ‘Phd’ ametoa rai kwa masanii wenganzake kutoa elimu juu ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa badaye mwezi huu badala ya wenyewe kuwa mashabiki wa vyama.
Pamekuwa na wimbi kubwa la wasanii tukumika kisiasa katika kipindi hiki cha kampeni kwa kinachodaiwa kuwa malipo makubwa hasa kutoka chama tawala.
Lakini badala ya kupanda kwenye majukwaa na kupigia kampeni upande mmoja katika uchaguzi huo, Phd ametaka watoe elimu ya upigaji kura.
Alisema asilimia kubwa ya wapiga kura mwaka huu ni wageni katika maswala ya upigaji kura , hivyo wanahitaji elimu ya kutosha.
“Nashangaa wasanii wenzangu badala ya kusimamia kwenye maswala ya upigaji kura, wao wamekuwa wa kwanza kutukna wagombea”, alisema.
Source: Lete Raha