Msanii Alikiba ametolea ufafanuzi wa post aliyoiweka Instagram na iliyozua mijadala na hisia tofauti kwa mashabiki wa muziki.
Akiongea na Diva katika kipindi “Ala za roho”, Alikiba amesema watu wameelewa tofauti post yake na ndio maana ameamua kuifuta.
“watu walinielewa vibaya mimi nilikua nawaambia mafans wangu, sababu wao ndio wananipigia kura mimi sikumaanisha kuhusu tuzo walinielewa vibaya,” alisema Kiba.
Pia King kiba alielezea sababu za kutompongeza msanii yoyote aliyeshinda tuzo hizo japo hata yeye mwenyewe alikua anawania, Kiba amesema kuwa hamna uzalendo.
“Siwezi ku-post kitu kuhusu kushinda kwao, unajua hakuna uzalendo. Watu wangapi wanafanya vitu vizuri hawapongezwi? Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo…unajua watu mimi hawanijui wanahisi kama mimi nina ringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda wasanii wote pia mziki mzuri,” aliongeza makli huyo wa Cheketua.
Pia Alikiba alisema kuwa hana tofauti yoyote na Diamond baada ya kuulizwa kuhusiana na uhusiano wao kwa sasa.
“Mimi sina tatizo na Diamond, nasikia kashida tuzo 3, nampongeza sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha kimataifa ni kitu poa sana…mimi na Diamond we are good,” alimaliza Alikiba.
print