Najua nina watu wangu ambao ni mashabiki wakubwa wa staa wa muziki kutoka Nigeria,Tiwa Savage… na pengine unajua ama hujui mengi sana kuhusu msanii huyo kutoka lebo ya Mavins Records ya Don Jazzy. Kama wewe ni miongoni wa mashabiki wakubwa wa Tiwa Savage basi hii ni kwa ajili yako mtu wangu.
Nimekutana na interview aliyofanya Tiwa Savage na jarida la Genevieve Magazine, toleo la mwezi November 2015 na humo ndani staa huyo amegusia vitu vingi ikiwa maisha ya ndoa, hali ya yeye kuwa mama na mambo mengine mengi.
Nimefanikiwa kuyakusanya machache aliyoyagusia Tiwa Savage na nimeona itakuwa poa nikishare na wewe baadhi ya mitazamo yake ya kimaisha…
Kuhusu kutokuwa na wapenzi wengi wakati wa ujana: “Hata kabla ya kuwa Mkristo, sikuwahi kuwa msichana wa namna hiyo. Kwenye familia yetu mimi ndio msichana pekee kati ya watoto wanne kwa hiyo nilizoea kuvaa mavazi ya kiume na nilikuwa sipendi kufanya vitu vya kike kama kutinda nyusi na kuvaa viatu virefu, mpaka leo sipendi kuvaa viatu virefu... Kwa hiyo hata akija mtu mwenye pesa vipi najua mume wangu ana imani siwezi kupagawa“
Vipi kuhusu imani ya kiroho: “Mimi ni mtu wa imani sana, nasali sana na huwa sina utani na mambo ninayozungumza na Mungu wangu.. japo sio kila wakati napiga goti na kusali lakini popote nitakapokuwa nahitaji nguvu au uwepo wa mungu, hata kama ni kwenye gari basi nitasimama na kuomba kwa Mungu wangu… Amenifanyia mengi sana na ninamuheshimu“.
Tutaiona lini sura ya mtoto?: “Huo ni uamuzi wa baba yake. Kila mzazi wa kike anapenda kila mtu aione picha ya mtoto wake. Binafsi natamani kuwaonyesha watu jinsi gani mwanangu alivyo mzuri sema nauelewa pia mtazamo wa mume wangu. Yeye ndio kichwa cha familia kwahiyo inanibidi niheshimu mitazamo yake pia. Ila very soon tutaiweka sura ya mtoto wetu hadharani, lakini kwa sasa ni ndugu na marafiki wa karibu ambao wamepata fursa ya kumuona mtoto“.