Leo watanzania wanaadhimisha miaka 17 toka Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amefariki dunia. Alifariki tarehe 14 Oktoba, 1999 huko Uingereza alipokuwa kwenye matibabu.
Kitaifa maadhimisho haya yanaenda sambamba na uzimwaji wa Mwenge wa uhuru Mkoani Simiyu, ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein Mkoani Simiyu.
Kwa upande wa staa wa muziki na filamu pamoja na wadau mbalimbali nchini, wameadhimisha siku hii kwa kuandika nukuu mbalimbali za Baba wa Taifa. Hizi ni baadhi ya nukuu.
Jokate Mwegelo
Happy Nyerere Day. Siku ya leo unamuenzi vipi baba wetu wa taifa?
Naomba nikuache na hii quote kutoka kwake. “Education is not a way to escape poverty, it is a way of fighting it”. Yaani, elimu ni nyenzo ya kupambana na umasikini sio nyenzo ya kukwepa umasikini. Kwa maana kama binadamu tuko duniani kupambana kuboresha mazingira yetu hilo halikwepeki lazima tule kwa jasho letu na elimu inatupa u-hodari na uelewa wa jinsi ya kupambana. “You can not develop people, you must allow people to develop themselves”. Kwa maana nyepesi Mwalimu alikuwa anasisitiza umuhimu wa kuweka mazingira yatakayomwezesha mtu kuwa independent in their thinking, kuweza kuibua kile alichowekewa ndani yake na Mungu kujiletea maendeleo yeye na jamii yake. Ndio maana binafsi sipendi shule za “spoon feeding” hazitengenezi vijana hodari na wenye kuweza kujiongoza wenyewe. Usengwile. #Tafakuru #Kidoti
Jux
Huwezi kuendeleza watu. lazima kuruhusu watu kujiendeleza wenyewe #mwalimujuliuskambaragenyerere #happynyerereday
Mrisho Mpoto
Kama mlango ukijiloki basi itafutwe njia ya Ku unlock hata kwa kuvunja, kama mlango umejibana basi itafutwe njia ya kuusukuma mpaka uwe wazi, lakini katika njia zote gharama za kuufanya mlango uwe wazi ziendane na kitu kilichopo ndani. Unandhani maneno haya yanamaana gani kwa hayati Mwl Julius Nyerere
Stereo
Washington are more important to us than those made here in Dar es Salaam. So, may be my people should be allowed to vote in American presidential elections.” (Julius Nyerere)