Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi mwakilishi wa kampuni ya Mount Cameroon. |
Mwakilishi kutoka kampuni ya kImori investment akiongea kea niaba ya washindi |
Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi, akiongea na wanahabari wakati wa hafla ya utoaji zawadi. |
Bajaji zilizotolewa kwa washindi wa usambazaji wa Bidhaa za SBL. |
Mwakilishi kutoka kampuni ya Smart builders akijaribu kuendesha bajaj aliyokabidhiwa kama zawadi. |
Waandishi wa habari wakishuhudia makabidhiano ya zawadi. |
Mwakilishi kutoka kampuni ya Kimori Investment akijaribu kuendesha bajaj aliyokabidhiwa kama zawadi mapema leo katika ofisi za makao makuu ya SBL Temeke Jijini Dar es salaam. |
Dar es Salaam, Oktoba 3, 2017 – Kampuni nne za usambazaji wa vinywaji kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Rukwa na Arusha zimejishindia bajaji moja moja yenye thamini ya shilingi 3.9m/- kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Kampuni hizo zimezawadiwa bajaji baada ya kuibuka wasambazaji bora wa bidhaa za SBL katika mikoa yao. Kampuni zilizoibuka washindi ni MM Group, Smart Builders, Kimori Investments NA Mount Cameroon inayofanya kazi katika mikoa ya Mbeya na Rukwa, Arusha na Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa hafala fupi ya kukabidhi zawadi hizo iliyofanyika Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmari amewapongeza washindi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuweza kushinda bajaji hizo zenye thamani ya jumla ya shilingi 15.6m/-
Mmasi amesema kampuni hizo nne zimeweza kuibuka washindi katika usambazaji wa pombe kali pamoja na bidhaa nyingine za kampuni hiyo zikiwamo bia.
Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kusambazwa na SBL ni pamoja na bia ya Serengeti, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Pilsner King, Kibo Gold, Guinness stout na Kick. Kampuni hiyo pia inasambaza pombe kali maarufu duniani kama Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.
“Tunawapongeza wasambazaji wetu hawa wanne ambao leo wameibuka washindi. Hii inaonyesha namna ambavyo wanafanya kazi kwa bidii na bajaji hizi zitawawezesha kufanya shughuli zao za usambazaji kwa urahisi zaidi,” alisema
Mmasi aliongeza kuwa zawadi kama hizo hutolewa na SBL kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kuwapongeza na kuwatia nguvu wasambazaji wake wanaofanya vizuri
Aliwataka wasambazaji ambao hawakuweza kuibuka washindi kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku akiwahakikishia kuwa zawadi zipo na kikubwa ni wao kuongeza jitihada
Mmasi aliwataka wasambazaji kufanya kazi kwa kushirikiana na kujituma lakini kwa ushindani ili pia waweze kushinda zawadi kubwa zaidi ambayo ni magari mapya aina ya Canter ambayo hutolewa wasambazaji wanaofanya vizuri kuliko wengine
Wakiongea wakati wa makabidhiano, wasambazaji hao wameshukuru SBL kwa kuwapa tuzo jambo ambalo wamesema litesaidia kukuwa kwa biashara zao huku wakiwataka wenzao ambao hawakufanikiwa kuibuka washindi kuongeza bidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kimori Investments Eden Kimori ambaye aliongea kwa niaba ya washindi wenzake alisema, motisha ya zawadi iliyoanzishwa na SBL imewafanya wasambazaji kufanya kazi kwa bidii zaidi
Alisema bajaji walizopewa zitawasaidia kuweza kufanya kazi ya usambazaji kwa urahisi zaidi na hivyo kuongeza mauzo yao.
Hii ni mara ya tatu kampuni ya SBL inawatunukia zawadi wasambazaji wanaofanya vizuri kwenye usambazaji wa bidhaa zake katika sehemu mbali mbali nchini. Mwezi Mei na Agosti mwaka huu, SBL ilitoa magari aina ya Eicher kwa sambazaji wake wa Katavi na Mwanza.