Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na Kikosi kazi cha kuzuia ujangili Tarehe 23 Februari 2024 Majira ya Saa Saba usiku katika maeneo ya Kijiji cha Mwamtani Bwawani Kata ya Mwamtani Tarafa ya Bumela Wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu likiwa katika doria za kupambana na uhalifu na wahalifu limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu ambao majina yao yamehifadhiwa wakiwa na vipande vitano (5) vya meno ya tembo yanayokadiliwa kuwa na uzito wa Kilo 60.
Akizungumza na waandishi wa habari Februari 23,2024 kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe alisema kuwa, Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutojihusisha na vitendo vya ujangili katika hifadhi za taifa zinazopakana na Mkoa wa Simiyu.
Aidha, Jeshi la Polisi linapenda kutoa pongezi kwa wananchi wanaondelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali.
#KonceptTvUpdates