Mahakama ya Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro imemuhukumu miaka 25 Jela Mawanga Prismus (42) Mkazi wa Kijiji cha Mavimba Tarafa ya Lupiro Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa kosa la Kupatikana na Nyara za Serikali.
Mtuhuniwa alikamatwa Mei 3, 2023 katika Kijiji cha Mavimba akiwa anauza nyama hiyo kwa wananchi akiisambaza kwa wateja wake kwa kutumia baiskeli ambapo amekutwa akiwa na Miguu mitatu ya Nyati pamoja na sikio.
Hukumu hiyo ilisomwa na Mh. Christopher Bwakila Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ulanga Machi 12, 2024.
#KonceptTvUpdates