WAKATI taifa la Tanzania likizidi kuzikumbuka nyimbo za marehemu Remmy Ongala, mtoto wa mwisho wa nguli huyo Tom Ongala, ameaumbia mtandao wa DarTalk kuwa baada ya kimya kidogo sasa anaratajia kuachia nyimbo inachokwenda kwa jina la ‘Week End’ ambayo kitakuwa zawadi kwa mashabiki wote waliokuwa wanamkubali baba yake.
Msanii huyo amekuwa ni mmoja wa watoto wa marehemu Ongala, anayefanya muziki alioachiwa na baba yake na mara nyingi amekuwa akipiga nyimbo za baba yake kwenye show zake.
Tom alisema kuwa anaamini kuimba kwake nyimbo za baba yake kunamfanya hata kwa upande wake kujizolea umaarufu kwa mashabiki wa baba yake kwani watu wengi bado wanazikubali kazi alizokuwa anafanya.
“Kwa sasa nipo katika mchakato wa kuingia studio ili kukamilisha nyimbo ya ‘Week End’ hivyo, nawaomba mashabiki wetu wajue kwamba bado muziki wa mzee unaendelea kuimbwa na kifo chake si kwamba hata nyimbo zake au staili yake ya muziki itakwua imekufa hapana bado tunaendeleza kile alichokiacha,” alisema