Na Prince
YANGA SC imetuma salamu Johannesrbug, Afrika Kusini ambako Azam FC wameweka kambi kujiandaa na msimu mpya- kufuatia ushindi wa mabao 5-1 leo katika mchezo wa kirafiki dhidi SC Villa ya Uganda, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga na Azam zitamenyana Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, katika mechi ya kuwania Ngao ya Jamii, kuashiria ujio wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam imeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na mechi hiyo ya kufungua msimu na Yanga wanaendelea na maandalizi yao Dar es Salaam, wakitarajiwa kuingia kambini baada ya mechi ya leo kisiwani Pemba, au Bagamoyo, Pwani.
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa 3-1, mabao yake yakifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya saba, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 27 na Didier Kavumbangu dakika ya 30, wakati la nne lilifungwa kipindi cha pili na Haruna Niyonzima dakika ya 62.
Bao la kufutia machozi la Villa ambayo jana ilifungwa 4-1 pia na Simba Uwanja huo huo wa Taifa, lilifungwa na Moses Ndaula dakika ya 18.
Katika mechi zake za awali za kujiandaa na msimu, Yanga SC ilitoa sare ya 2-2 na URA ya Uganda kabla ya kuzifunga 3-1 Mtibwa Sugar na 3Pillars ya Nigeria 1-0.
Azam nayo imekwishacheza mechi tatu za kujipima nguvu Afrika Kusini, imeshinda moja tu dhidi ya Mamelodi Sundwons 1-0, imefungwa mbili, 3-0 na Kaizer Chiefs na 2-1 na Orlando Pirates na kesho itacheza mechi ya mwisho na Moroka Swallows kabla ya kurejea nyumbani keshokutwa.
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David Luhende/Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Rajab Zahir, Athumani Iddi ‘Chuji’/Bakari Masoud, Mrisho Ngassa, Salum Telela, Didier Kavumbangu, Jerry Tegete/Hussein Javu na Haruna Niyonzima/Said Bahanuzi.

Akaunti mpya; Ngassa amefungua akaunti mpya ya mabao Yanga leo |

CHANZO; BIN ZUBEIRY