William Masvinhu kwa mara nyingine tena amenyakua taji la Mwenye Sura
Mbaya huko Zimbabwe katika shindano lililofanyika siku ya Ijumaa ndani
ya ukumbi wa City Sports Bar.
Amepewa taji, hela pamoja na Ofa ya mwanae mmoja kulipiwa ada ya shule
kwa mwaka mmoja, mke wake William naye alikuwepo ukumbuni hapo na
alifurahia sana ushindi huo wa mumewe.
Katika kujifaharisha na taji lake, William alisema” Ubaya wa Sura yangu
ni wa Asili, ingawa nilijiaanda kidogo kwa shindano hili lakini mengine
niliyaacha yajishughulikie yenyewe”
Hao ndio washiriki wote kwa ujumla ambapo William alitoka Kidedea |