Na Khatimu Naheka
MUDA mfupi baada ya kumalizika
kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Kocha wa Yanga, Ernie Brandts
ameliambia gazeti hili kuwa, anaondoka kuelekea kwao Uholanzi lakini
hajasaini mkataba mpya Yanga.
Akizungumza na Championi Ijumaa muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya
JKT Oljoro uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Brandts alisema
amelazimika kuondoka haraka kuiwahi familia yake ili kuweka mambo sawa
kuhusu familia yake.
“Naondoka muda mfupi kutoka sasa (jana usiku), narudi nyumbani mara
moja, kuna mambo natakiwa kwenda kuyafanya kule, kuhusu kusaini bado
sijafanya hivyo, nafikiri tusubiri kwa sababu sijajua mpango wa viongozi
wa klabu,” alisema Brandts.
Aidha, kocha huyo amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo baada ya
kusema atarudi nchini mapema kwa lengo la maandalizi ya kikosi chake
hicho kitakachoanza majukumu ya mechi za Klabu Bingwa Afrika mapema
mwakani.
CHANZO; GPL