Lucy Mgina na Martha Mboma
KOCHA wa Simba,
Abdallah ‘King’ Kibadeni, amesema anahitaji kuongeza wachezaji katika
safu ya ulinzi wa kati pamoja na kipa mwenye kiwango cha juu.
Tamko hilo linakuja wakati ambapo Simba imekuwa ikimtumia Mganda,
Abel Dhaira kama chaguo la kwanza na Abuu Hashim akiwa msaidizi wake
wakati Andrew Ntalla aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar akipoteza nafasi
kutokana na kuonyesha kiwango cha chini.
Kibadeni ameliambia gazeti hili kuwa, amebaini makosa katika safu ya
ulinzi wa kati, hivyo ni lazima aingie sokoni katika usajili wa dirisha
dogo kwa ajili ya kusaka vifaa watakaoziba nafasi hiyo.
Akimzungumzia Dhaira, kocha huyo alisema Mganda huyo amekuwa
akiruhusu mabao mepesi, hali iliyosababisha kuamua kumpa nafasi Abuu
ambaye naye aliruhusu mabao matatu katika michezo mitatu.
“Nashukuru licha ya kuwatumia vijana wengi msimu huu wameonekana
kupigana na kusaidia kumaliza mzunguko wa kwanza katika nafasi hii ya
tatu,” alisema Kibadeni.
CHANZO; GPL